KIDDIE JUNCTION SONGWE AIRPORT AND IFISI ZOO STUDY TOUR 2025
Watoto walipata nafasi ya kutembeleamaeneo mawili muhimu ya kutalii na kujifunza kwa vitendo.
Ifisi zoo waliona wanyama wa porini kama Simba, Fisi, Chatu, Mbuni na wanyama wengine.
Walipata nafasi ya kukutana na kupiga picha ya pamoja na Spika wa Bunge, na rais wa Mabunge Duniani.
Kutalii na kujifunza kwa vitendo ni sehemu ya masomo yanayozingatiwa zaidi katika shule zetu za msingi na elimu ya awali, kwani tunatambua watoto wadogo wanajifunza zaidi kwa kuona vitu hivyo inawasaidia kukuza uelewa wao na kuwakuza ki taaluma.
Kwa kulizingatia hilo tumekua na utaratibu wa kuwatoa watoto maeneo tofauti yanayokuwa rafiki kwa kujifunza na kutalii mara kwa mara na msimu huu watoto walitembelea hifadhi ya wanyama ya ifisi na uwanja wa ndege wa songwe kujifunza kwa vitendo.
katika ziara hii watoto wetu wakiwa Uwanjani hapo walipata nafasi ya kuonana na aliyekua Spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na rais wa mabunge duniani Mhe. Dr. Tulia Akson na kupiga nae picha ya pamoja.
Kutazama picha na video tembelea Kurasa zetu za youtube @ kiddie junction day care academy kwa kubonyeza kiambata (link) hapa chini....